Wanaharakati Mombasa yalalamikia polisi baada ya kifo cha Susan Mito

by KenyaPolls

Watetezi wa haki za binadamu Mombasa wamekashidi Idara ya Usalama kwa utepetevu wa kazi, baada ya kifo cha Susan Achieng Mito, mwanaharakati wa maswala ya kijinsia, aliyepigwa kisu tumboni na mumewe tarehe 5 Aprili, 2026, na kufa baada ya kugaliwa hospitalini kwa siku kumi.

Polisi wamekashwa kwa kutochukua hatua baada ya Susan kuripoti vitisho kutoka kwa mtumaji hatua. Pia, wanaharakati wamesikitikia huduma alizopata hospitalini, baada ya madai ya kunyimwa ombi la kuhamishwa hospitali kubwa.

Wakiongozwa na Zedekiah Adika na wakili wa familia Terry Mwongeli, kundi hilo limeomba uchunguzi wa kina, na kuwajibishwa maafisa wa polisi na wahudumu wa afya walioshughulikia kesi hiyo ikiwa watapatikana na hatia.

Adika alisema: ”Ripoti kuhusu vitisho dhidi ya maisha yake ilisababishwa katika kituo cha polisi tarehe 2 Machi na dadake, huku yeye mwenyewe akaripoti baada ya mshukiwa kuchoma bidhaa zake. Tunashangaa kwa nini mshukiwa aliachwa huru. Tunahisi polisi hawakuwajibika vizuri, na tunataka kujua misingi gani mshukiwa aliachiwa huru licha ya madai hayo, na baadaye tutawasilisha malalamisi mahakamani.”

Dadake marehemu Emily Mito ameelezea huzuni ya familia kufuatia kumpoteza mpendwa wao, na ametaka haki itendeka.

”Wanawake wanaopitia dhulma za kijinsia wanaamini wapata msaada wakipiga ripoti polisi. Tungeomba Idara ya usalama iwasaidie kwa namna inavyostahili. Katika kesi hii, tunaona kulikuwa na ulegevu, kwa sababu hakuna hatua iliyochukuliwa.”

Chama cha Wanasheria Wanawake Nchini (FIDA) kimetangaza kesi 15 za dhulma za kijinsia katika ukanda wa Pwani mwaka huu, hali inayoibua wasiwasi kuhusu usalama na haki za wanawake.

Wakili Terry Mwongeli ameitaka serikali ya Mombasa kujenga kituo cha kuhifadhi waathiriwa, kubaji ya kuwasaidia, na kutekelezwa mapendekezo ya ripoti ya jopo la kukabiliana na ongezeko la mauaji wa wanawake na ukatili wa kijinsia.

Hata hivyo, mshukiwa alikamatwa na kufikishwa mahakamani tarehe 14 Aprili, ambapo Mahakama ya Mombasa iliamuru azuiliwe kwa siku 17, uchunguzi ukiendelea.

Marehemu ameacha watoto wawili wa kiume wenye umri wa miaka 19 na 11.

You may also like